WANAMGAMBO WAKAMATWA IRAQ
23 Desemba 2003Matangazo
BAQUBA: Askari jeshi wa Kimarekani nchini Iraq wamewakamata wanamgambo watatu wa kiislamu wenye uhusiano na msaidizi mkuu wa zamani wa Saddam Hussein- Izzat Ibrahim al-Douri.Katika orodha ya Wairaqi 55 wanaosakwa na Marekani,al-Douri ni namba 6.Kuna zawadi ya Dola milioni 10 kwa ye yote yule atakaetoa habari zitakazomkamatisha msaidizi huyo wa zamani wa Saddam Hussein.Inaaminiwa kuwa al-Douri ndio huongoza upinzani dhidi ya Wamarekani nchini Iraq.Wanamgambo hao watatu wamekamatwa siku moja tu baada ya kukamatwa Mumtaz al-Taji aliekuwa jemadari mkuu katika idara ya upelelezi.