Wanamgambo wa RSF wazishambulia hospitali El-Obeid
30 Mei 2025Matangazo
Haya ni kwa mujibu wa mashuhuda na chanzo cha kijeshi. Haya yanafanyika wakati ambapo jana, wanamgambo hao walisema wameuteka tea mji wa Al-Khoei ulioko karibu kilomita 100 magharibi mwa El-Obeid, baada ya kuchukuliwa na jeshi mapema mwezi huu.
El-Obeid, mji wa kimkakati ulioko kilomita 400 kusini magharibi mwa Khartoum, ndio mji mkuu wa jimbo la North Kordofan, na ulivamiwa na wanamgambo wa RSF kwa karibu miaka miwili kabla jeshi la Sudan halijawafurusha wanamgambo hao na kuchukua udhibiti mwezi Februari.
Hiyo ilikuwa mojawapo ya mashambulizi ya jeshi yaliyolipelekea kuuteka tena mji wa Khartoum mapema mwaka huu ila mji huo mkuu umeendelea kushambuliwa kwa mabomu na RSF.