MigogoroUturuki
Kundi la PKK latangaza usitishwaji mapigano nchini Uturuki
1 Machi 2025Matangazo
Uamuzi huo unakuja siku mbili baada ya kiongozi wao aliyeko jela tangu mwaka 1999 Abdullah Ocalan, kutoa wito kwa wapiganaji wa kundi hilo kuweka chini silaha.
Taarifa ya Chama cha Kikurdi, PKK, imesema usitishaji mapigano unaanza kutekelezwa leo Jumamosi kama njia ya kuitikia wito wa Kiongozi wao kwa ajili ya amani na uwepo wa jamii ya kidemokrasia na kusisitiza kuwa wapiganaji wao hawatochukua hatua zozote za kivita isipokuwa wakishambuliwa.
Mzozo kati ya Uturuki na chama cha PKK, kilichopigwa marufuku nchini humo, ulianza mwaka 1984 na umesababisha vifo vya maelfu ya watu, huku uwepo wa kundi hilo nchini Iraq, kikiwa chanzo cha migogoro ya mara kwa mara kati ya serikali mjini Baghad na Uturuki.