Wanajeshi wanaofuata siasa kali wafukuzwa Bundeswehr
26 Agosti 2025Matangazo
Tayari jeshi la Ujerumani limeshawafukuza wanajeshi 90 baada ya kuthibitishwa kuwa na misimamo ya siasa kali za mrengo wa kulia mnamo mwaka jana.
Wizara ya ulinzi Ujerumani, ambayo ilikuwa ikijibu maswali kwenye uchunguzi wa kamati ya bunge kutoka kwa wanachama wa chama cha mrengo wa kushoto, imesema jumla ya matukio 280 ya mitizamo ya siasa kali za mrengo wa kulia yalithibitishwa miongoni mwa maafisa wa kijeshi mwaka jana.
Chama cha mrengo wa kushoto, Die Linke, kimesema ongezeko la wanajeshi wenye kufuata mrengo wa siasa kali linatisha.