Wanajeshi wawili wengine wa Kimarekani wauawa Iraq:
13 Machi 2004BAGHDAD: Nchini Iraq wameuawa wanajeshi wawili wengine wa Kimarekani. Wanajeshi watano wengine walijeruhiwa katika shambulio hilo lililofanywa katika kitovu cha mji wa Tikrit, aliarifu msemaji wa kijeshi wa Kimarekani. Shambulio hilo lilifanyika wakati wa safari ya ukaguzi katika mji huo uliyoko Kaskazini mwa mji mkuu Baghdad. Kufuatana na ukumbusho wa mwaka wa kwanza wa kuanza Vita vya Iraq wapinzani wa vita kutoka kila sehemu ya Marekani wanajiandaa kufanya maandamano makubwa mjini Weashington. Inasemekana maandamanio hayo katika mji mkuu wa Marekani yataanzia mbele ya hospitali ya kijeshi ambako mara kwa mara hupepelekwa maiti za wanajeshi wa Kimarekani waliouawa Iraq. Hadi sasa wamekwisha uawa zaidi ya wanajeshi 550 wa Kimarekani nchini Iraq.