Wanajeshi wawili watiwa na hatiani na ukatili waliofanya Iraq.
24 Februari 2005Wanajeshi wawili wa Uingereza wamepatikana na hatia ya kuwafanyia vitendo vya ukatili raia wa Iraq,wakati mwengine wa tatu ametiwa hatiani kwa kushindwa kutoa ripoti ya kufanyika kwa vitendo hivyo.Mahakama ya kijeshi iliyowatia hatiani wanajeshi hao ilikutana katika kituo cha kijeshi cha Uingeraza kilichopo mjini Osnabrueck hapa Ujerumani.Hata hivyo hukumu kwa wanajeshi hao imeahirishwa hadi kesho Ijumaa.
Matukio hayo ya vitendo vya ukatili yalifanyika mwaka 2003 baada ya wanajeshi wa Uingereza kuwazunguka watu waliokuwa wakifanya uporaji katika ghala moja mjini Basra kusini mwa Iraq.
Ushahidi kuhusiana na tuhuma hizo uliibuliwa baada ya mwanajeshi wa nne kuchukua picha za vitendo hivyo vya ukatili na baadae kuzipeleka kusafishwa katika studio ya nyumbani kwao Uingereza.Baadaye mfanyakazi wa studio hiyo alipoziona picha hizo aliwaarifu polisi.