Wanajeshi watatu wa Kenya wauawa karibu na mpaka na Somalia
16 Julai 2025Matangazo
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne jioni, jeshi hilo limesema kuwa msafara wa wanajeshi hao liligonga kilipuzi hapo jana katika barabara kati ya Sankuri na Kiunga, mji wa Pwani ulioko umbali wa kilomita 12 kutoka mpaka wa Somalia.
Al Shabaab yawaua maafisa sita wa polisi nchini Kenya
Pia limesema limesikitishwa na vifo vya wanajeshi hao shupavu.
Wakati huo huo kupitia tovuti yake, kundi linalojiita dola la kiisalmu IS lenye mafungamano na al-Qaeda, limethibitisha kuuawa kwa wanajeshi wawili wa Kenyakatika mlipuko uliolenga msafara katika eneo kama hilo jana Jumanne lakini halikudai kuhusika moja kwa moja.