Wanajeshi watano wa Israel wauawa Ukanda wa Gaza
8 Julai 2025Matangazo
Wanajeshi wengine 14 wamejeruhiwa, na wawili kati ya hao wako mahututi. Vifo vya wanajeshi wa Israel vimetokea baada ya kulipukiwa na bomu lililotegwa kando ya barabara ikiwa ni wiki mbili baada ya wanajeshi wengine saba kuuawa kwa bomu lililotegwa kwenye gari lao la kivita.
Hayo yanajiri wakati mamlaka za Palestina zikisema watu 18 wameuwawa kwa mashambulizi ya Israel. Moja ya mashambulizi yaliyoulenga mji wa Khan Younis limewauwa watu wanne wa familia moja, wakiwemo mama, baba, na watoto wao wawili.