WANAJESHI WA UITALIA WAUAWA IRAQ:
13 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Si chini ya Wataliana 18 na Wairaqi 8 wameuawa mjini Nassriya kusini mwa Iraq,katika shambulio kubwa lililofanywa dhidi ya makao makuu ya vikosi vya Kitalana.Shambulio hilo la kujitolea mhanga maisha limewajeruhiwa pia zaidi ya watu 100.Kwa sababu ya shambulio hilo,raia wa Kitalaina mjini Roma wametoa muito wa kuwarejesha nyumbani wanajeshi wao 2,400 walio nchini Iraq,lakini waziri mkuu Silvio Berlusconi amesema Italia haikubali kutishwa.Hispania,Ureno na Poland vile vile zimekula kiapo kuwa vikosi vyao vya wanajeshi 6,000 vitabakia nchini Iraq kama sehemu ya muungano unaoongozwa na Marekani.