Wanajeshi wa Uingereza waokolewa Irak
20 Septemba 2005Matangazo
Basra:
Wanajeshi wa Uingereza wamewaokoa Wanajeshi wenzao wawili waliokamatwa na polisi wa Irak mjini Basra baada ya kutekwa nyara na Wanamgambo wa Kishia. Kamanda wa kikosi cha 12 mjini Basra, Brigedia John Lorimer, amesema kuwa Wanajeshi hao wameokolewa kutoka nyumba moja mjini humo ambako walikuwa wamefichwa na Wanamgambo hao. Ameongeza kusema kuwa watafuatilia kwa nini wakuu wa Basra hawakuwakabidhi haraka Wanajeshi hao kwa majeshi ya kimataifa kama vile sheria za Irak zinavyoamuru. Maafisa wa Irak wamesema kuwa Wanajeshi hao, walioelekea kuwa askari kanzu, walivaa mavazi ya Kiarabu na kuendesha motokaa ya kiraia. Wamekamatwa baada ya kufyatulia risasi doria ya polisi.