Wanajeshi wa Uganda wakamatwa Kenya kwa madai ya thuluma
6 Februari 2025Matangazo
Kwa muda mrefu, wavuvi wa Kenya wamelalamikia dhuluma kutoka kwa maafisa wa Uganda, ikiwemo kuporwa nyavu na kulazimishwa kula samaki wabichi.
Tukio hilo limepokelewa kwa shangwe na wavuvi wa Kenya, ambao wanaitaka serikali yao kuanzisha mazungumzo na Uganda ili kupata suluhisho la kudumu kuhusu uvuvi kwenye Ziwa Victoria.
Jeshi la Uganda kuimarisha ulinzi katika eneo la Mashariki mwa Kongo
Hadi sasa, serikali ya Uganda haijatoa tamko lolote kuhusu kukamatwa kwa wanajeshi wake. Kamishna wa Busia, Chaunga Mwachaunga, anatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu hatma ya wanajeshi hao.
Haya yanajiri huku afisa mwingine wa UPDF akiendelea kuzuiliwa katika gereza la Korinda, Busia, kwa kumuua mvuvi wa Kenya mwaka uliopita kwenye Ziwa Victoria.