UhalifuNigeria
Wanajeshi wa Nigeria wawaua wiki hii majambazi wapatao 150
11 Julai 2025Matangazo
Hayo yameelezwa Alhamisi na afisa wa eneo hilo Husaini Bena aliyeongeza kuwa wanajeshi walivizia msafara mkubwa wa majambazi walipokuwa wakipita katika vijiji vya jimbo la Kebbi katika wilaya ya Danko-Wasagu siku ya Jumatano, na kuzusha mapigano yaliyodumu kwa masaa mawili.
Majambazi hao waliokuwa kwenye msafara wa karibu pikipiki 350, walikuwa wakielekea katika kambi yao katika taifa jirani la Niger. Kwa miaka kadhaa sasa, magenge ya utekaji nyara na yenye silaha nzito yamekuwa yakizidisha mashambulizi katika maeneo ya kaskazini-magharibi na katikati mwa Nigeria na kuua maelfu ya watu.