Wanajeshi wa Kimarekani washambuliwa Iraq:
25 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq mwanajeshi mmoja wa Kimarekani alifariki baada ya kujeruhiwa hapo jana msafara wa magari ya kijeshi ya Kimarekani uliposhambuliwa katika safari yao kutokea Baghdad kuendea Beishi, Iraq ya Kaskazini. Hivi sasa kimefikia 513 kiwango cha wanajeshi wa Kimarekani waliouawa Iraq tangu vimalizike rasmi vita. Hapo jana waliuawa jumla ya wanajeshi watano wa Kimarekani katika orodha ya mashambulio nchini Iraq.