MigogoroPakistan
Wanajeshi 18 wauawa Pakistan katika mapambano na wanamgambo
1 Februari 2025Matangazo
Taarifa ya jeshi iliyotolewa Jumamosi imebainisha kuwa mapigano hayo yalizuka kwenye mkoa usio na utulivu wa Balochistan, baada ya wanamgambo kuweka vizuizi katika barabara kuu, na ndipo jeshi lilianzisha operesheni kadhaa za kuviondoa vizuizi hivyo.
Wanamgambo 12 waliuwawa katika wilaya ya Kalat na 11 kwenye wilaya ya Herani. Kundi la wanamgambo la Baloch Liberation Armylimekiri kuwa ndilo lililohusika na mauaji ya wanajeshi kwenye mapambano hayo, lenyewe likidai limewauwa wanajeshi 17 pekee tofauti na takwimu za jeshi.
Mashambulizi mengi katika mkoa wa Balochistan yamekuwa yakiilenga miradi ya miundombinu ya China yenye thamani ya mabilioni ya dola.