Wanaharakati wataka kushawishi makubaliano ya plastiki
12 Agosti 2025Wanaharakati hao wanayataka mataifa yaonyeshe ujasiri na kusaini makubaliano yenye nguvu.
Idadi kubwa ya waandamanaji hao walikuwa wanatokea vuguvugula Break Free From Plastic wakisema wanataka sauti zao zisikike huku mazungumzo hayo ya Uswisi yakiwa yanaelekea kufikia mwisho.
Mataifa huko Uswisi yanabuni makubaliano ya kwanza ya uchafuzi wa mazingira kwa plastiki yanayozifunga kisheria nchi duniani.
"Tumewekeza sana kuja kote huku Geneva, mbali na jamii zetu, mbali na familia zetu, kwasababu tunaelewa jinsi jambo hili lilivyo muhimu na jinsi muda huu ulivyo muhimu, ni makubaliano ya plastiki ambayo hayatushuhudiwa tena maishani," alisema Juressa Lee, mwanaharakati kutoka New Zealand.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufikia mwisho siku ya Alhamis.