Wanafunzi warejea shuleni katika mazingira magumu Goma
1 Septemba 2025Kwenye miji ya Goma na Bukavu, wazazi wengi wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kuwaandaa watoto wao kwa mwaka mpya huu wa shule. Ingawa hii tarehe mosi Septemba wanafunzi wamerudi shule kama ilivyopangwa na Wizara ya Elimu, hali ya kiuchumi inazidi kuwa mbaya,kama wanavyo bainasha wazazi hao.
"kuanzishwa kwa shughuli za shule, hatuna matumaini kwamba tutaweza sababu maisha ni mazitu sana,hakuna ajira tunafanya kazi ndogondogo lakini sio rahisi sababu benki zimefungwa. ombi letu kwa wakuu viongozi nikufungua Benki ili tuona kwamba watoto wetu wanaweza rudi shule".
Kutokana na kukwama huko kwa huduma za benki ni sasa zaidi ya miezi nane, wazazi wengi hawawezi kupata fedha za kuwahudumia watoto wao. Hali hii imeongeza wasiwasi miongoni mwa familia nyingi, huku ukosefu wa usalama ukiathiri maisha yao ya kila siku. Hii juma tatu ni idadi ndogo ya watoto walikua waliovalia sare za shule ndio walionekana kwenye shule zao tafauti na kama ilivyokuwa kawaida ,amesema bwana Nyiringiye Jonas kiongozi wa shule Ushindi ,katikati mwa mji wa Goma.
"Tumewashukuru viongozi wa serikali kuruhusu kuanzishwa kwa mwaka wa shule lakini bado wazazi wamoja wanamasito , sababu ya usalama na wengine ,uhaba wa pesa.Matumaini yetu nikuona wiki hii watoto wote wamewasili shuleni. "
Katika tangazo lao mwishoni mwa juma iliyopita,viongozi wa kundi la AFC/M23 wanaozishikilia miji ya Goma na Bukavu,walieleza nia yao yakusindikiza shughuli zote za elimu katika maeneo wanayo yatawala jambo ambalo linatizamwa na wananchi kama kitendawili.
Hata hivyo, baadhi ya wazazi wanataja matatizo kama vile kukosa uwezo wa kununua vifaa vya shule, malipo ya ada, na hata mahitaji ya msingi kama chakula.
"nimetuma watoto wawili lakini moja amebaki nyumbani sababu sina uweza ,vita vimegusa maisha yangu kabisa. "
Hii ni hali inayo athiri kasi ya elimu kwa watoto hawa ambao wengi ni waathirika wa vita.
Taarifa kutoka kwa viongozi wa mitaa inaonyesha kuwa watu wengi wanatarajia mabadiliko katika huduma za benki ili kuweza kujiandaa kwa mwaka mpya wa shule huku wakiomba serikali kuchukua hatua za haraka ili kuboresha hali hii.