Wanafunzi wa Ujerumani wanazingatia mambo ya Afrika
7 Novemba 2005Vipi unaweza kupambana na rushwa ikiwa huwezi kuwadhibiti wanasiasa? Nchi za Kiafrika zenyewe zina uwezo gani wa kupambana na umaskini? Na msaada wa aina gani unataka kupewa na Ulaya?
"Kweli, haya ni maswali magumu", anasema Paul Fokam, mtaalamu wa uchumi kutoka Kamerum. Halafu akawaeleza wanafunzi wa Ujerumani mawazo yake ya kuisaidia Afrika kujiendeleza. Ndiyo, lazima nchi za Magharibi zitoe michango yao, lakini kwa kuweka masharti yenye hakika. Hasa elimu ipewe umuhimu, lakini siyo kujenga majengo mapya lakini kuwaelemisha walimu.
Mada zilizozungumzwa katika mkutano huo mdogo kati ya wanafunzi 30 na wajumbe watano wa Afrika zilikuwa za umuhimu kufikia hizo za mkutano rasmi wa Rais Horst Köhler. Kwa mfano, wanafunzi wa umri wa miaka 17 au 18 walioshiriki majadiliano hayo walivutiwa sana na Umoja wa Afrika, kwani kifanani chake, yaani Umoja wa Ulaya una uhuminu mkubwa nchini Ujerumani.
Kwa nini, vijana waliuliza, Umoja wa Afrika hauwezi kutatua mzozo baina ya Ethiopia na Eritrea juu ya mpaka wao? Anayelijibu swali hilo ni John Makumbe, mwenyekiti wa tawi la shirika la kupambana na rushwa Transparency International nchini Zimbabwe, ambaye pia anahusishwa na Umoja wa Afrika kutochukua hatua kali dhidi ya rais wa nchi yake, Robert Mugabe. Bw. Makumbe anaeleza: „Umoja wa Afrika bado ni mtoto, ni mtoto mchanga. Bila msaada kutoka nje hauna na uwezo wa kuzitekeleza sheria zake. Umoja wa Ulaya unaweza kutusaidia lakini kwa njia inayofaa. Maanake, siyo kwa kutoza kiwango cha Ulaya lakini kwa kuleta msaada wa ushirikiano. Siyo lazima msaada huo ni kupeleka wanajeshi wa Ufaransa au Uingereza barani Afrika, lakini ni kuyasaida mataifa ya Afrika kujisaidia ili hayalazamishwi kutumia fedha zinazohitajika hupiga vita umaskini katika nchi hizo. – mwisho wa kumnukuu John Makumbe.
Wanafunzi wa Ujerumani hawakujifunza ujuzi wao wa kuzungumzia mada kama siasa au uchumi shuleni. Badala yake walishiriki katika warsha maalum iliyoandaliwa na taasisi ya taifa ya kutoa mafunzo ya kisiasa ya Ujerumani kabla ya majadiliano wa mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa miaka mitatu taasisi hiyo inazingatia masomo maalum kuhusu mambo ya Kiafrika, kwa sababu mambo haya hayafundishwi sana shuleni. Mwanafunzi mmoja anaeleza, yuko katika darasa la mwisho, lakini mpaka sasa alipata masomo mawili tu kuhusu historia ya kikoloni barani Afrika. Haya anasema, hayatoshi kabisa.
Mwingine analalamika kuwa alijifunza tu kidogo kuhusu msitu wa mvua na uchumi barani Afrika, lakini siasa ya mambo ya maendeleo haizungumziwi. Wanafunzi hawafahamu Afrika kwa sababu ya mfumo wa elimu nchini Ujerumani.
Lakini siyo tu mfumo wa elimu, bali pia vyombo vya habari havitoi taarifa za habari za kutosha zinazohusu Afrika. Hata hivyo, kwa kuwapa tu masomo machache zaidi pamoja na kukutana na wajumbe kutoka nchi za Afrika wenyewe iliwavutia sana vijana. Mwisho wa mkutano huo wengi wao walijiuliza: Vipi naweza kutoa mchango wangu?
Kwa mujibu wa Paul Fokam kutoka Kamerun siyo lazima iwe mchango wa fedha. Alisema: "Kwangu mimi, hasa ni tatizo la mashaka na tatizo la kutokuwa na mustakabali. Je, nataka kujitolea ili mambo yabadilishwe? Je, nataka kuyaondoa mashaka yangu? Je, naamini kwamba siku za usoni za bara la Afrika zinahusiana pia na wakati wangu wa mbele? Haya ningependa yazungumziwe katika shule za nchi za magharibi."