MigogoroMashariki ya Kati
Wanadiplomasia wa Ulaya kukutana na mwenzao wa Iran
20 Juni 2025Matangazo
Mawaziri hao Johann Wadephul wa Ujerumani, Jean-Noël Barrot wa Ufaransa na David Lammy wa Uingereza watakutana na Abbas Araghchi wa Iran wakiwa pamoja na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas.
Mkutano huo unafanyika katikati ya mapigano baina ya Israel na Iran yaliyozuka mnamo wiki iliyopita baada ya Israel kuishambulia Iran ikisema imechukua hatua za kijeshi dhidi ya mradi wa nyuklia wa nchi hiyo.
Israel pia imekuwa ikimrai Rais Donald Trump wa Marekani kuishambulia miundombinu ya nyuklia ya Iran wanayoituhumu kuwa na mpango wa kuunda silaha za nyuklia, madai ambayo Tehran imeyakanusha kila wakati.