Wanachama wa B9 wako tayari kuipokea Ukraine NATO
2 Juni 2025Nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO za kanda ya Nordic,Baltic na za Ulaya ya kati zimesema ziko tayari kuipokea Ukraine kuwa mwanachama wa muungano huo.
Viongozi wa Poland,Romania na Lithuania wametoa mtazamo huo kupitia taarifa yao ya pamoja baada ya mkutano wa kilele wa kile kinachoitwa kundi la B9 na nchi za Nordic.
Rais Volodymyr Zelensky ambaye pia anashiriki mkutano huo mjini Vilnius amezungumzia juhudi za kidiplomasia zilizofanyika Istanbul,Uturukikwa kutoa kauli hii, tunanukuu:
"Tunapaswa kufanya kila kitu kuhakikisha diplomasia haitoki patupu.Ujumbe wetu hivi sasa uko Istanbul na tuko tayari kuchukua hatua zinazohitajika kufikia amani.Bila shaka mwanzo unatakiwa kuwa ni usitishaji vita na uendeshaji shughuli za kibinadamu,kuachiwa wafungwa na kurudisha watoto Wakiukraine waliotekwa.Na mambo yote muhimu yanaweza kutatuliwa katika ngazi ya viongozi.'' Mwisho wa kunukuu
Zelensky pia amewaambia viongozi wanaokutana, kwamba ikiwa rais Putin atahujumu juhudi za Istanbul,watapaswa kumuwekea vikwazo.
Viongozi kwenye mkutano huo wa Vilnius wanatarajiwa pia kuzungumzia kuhusu kuipatia Ukraine uungaji mkono zaidi wa kijeshi na kisiasa.