Wanaanga waliokwama angani kwa miezi 9 warejea duniani
19 Machi 2025Matangazo
Wanaanga wawili wa Shirika la Marekani la Sayansi na Teknolojia ya Angani. NASA, hatimaye wamerudi duniani usiku wa kuamkia leo baada ya kukwama angani kwa miezi tisa. Butch Wilmore na Suni Williams pamoja na Mmarekani mwenzao Nick Hague na mwanaanga wa Urusi Aleksandr Gorbunov walitua baharini huko Florida huku wakishangiliwa na kundi la watu.
Soma:SpaceX yafanya jaribio la pili la roketi la Starship
Wanaanga hao 4 waliondoka duniani mwezi Juni mwaka jana katika safari ya kwenda angani kwa siku chache tu, ila chombo kilichowabeba kilipata matatizo ya kiufundi na kudaiwa kuwa hakiko salama kuwarejesha duniani na kikaishia kurudi kitupu. Walisalia angani kwa miezi tisa.