Wanaanga wa Marekani na Urusi warejea salama duniani
20 Aprili 2025Matangazo
Kwa mujibu wa shirika la anga za juu la Urusi Roscosmos na shirika la anga za juu la Marekani NASA chombo kilichowabeba wanaanga hao, Don Petit Alexei Ovchinin na Ivan Wagner kilitua Asubuhi kwenye eneo la nyika za Jamhuri ya Asia ya Kati ya Kazakhstan.Petit anasherehekea miaka yake 70 ya kuzaliwa leo hii. Kwa mujibu wa NASA wanaanga hao wamekuwa katika anga za juu tangu Septemba 11. Licha ya mvutano mkubwa wa kisiasa wa kimataifa kufuatia vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, Urusi na Marekani zimekuwa zikiendelea kufanya kazi pamoja linapokuja suala la uchunguzi wa anga.