Wakuu wa SADC wakutana Harare kuujadili mzozo wa Kongo
31 Januari 2025Matangazo
Kikao hicho kisicho cha kawaida kinachokutanisha mataifa 16 kimeitishwa baada ya waasi wa M23 wiki hii kukamata eneo kubwa la mji wa Goma na kuibua wasiwasi juu ya usalama wa kikanda.
Wanajeshi 13 kutoka Afrika Kusini na watatu wa Malawi wameuawa kwenye mapigano yaliyoanza Ijumaa iliyopita, wengi wao wakiwa ni sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa SADC ulioepelekwa kwenye eneo hilo mwaka 2023.
Soma pia:UN yaelezea wasiwasi kuhusu M23 kusonga mbele Bukavu
Rwanda inayoshutumiwa kuwaunga mkono M23, sio mwanachama wa SADC, lakini Kongo ni mwanachama.