Wakuu wa makampuni makubwa makubwa ya ujerumani watakiwa wachapishe kiasi gani wanapata kwa mwaka
18 Mei 2005Matangazo
Wakuu wa makampuni makubwa makubwa ya Ujerumani yanayoshiriki katika soko la hisa,watalazimika kuanzia mwakani kuchapisha mishahara yao na marupu rupu wanayopokea.Baraza la mawaziri limepitisha mswaada huo wa sheria hii leo. Makampuni kama elfu moja hivi yanahusika na sheria hiyo mpya.Kwa namna hiyo serikali ya shirikisho inataka kuwarahishia mambo waweka hisa, kuona kama kweli mameneja wanapokea mishahara mikubwa mikubwa kuliko kazi yenyewe wanayofanya.Kwa mujibu wa waziri wa sheria Birgitte ZYPRIES mameneja watakaopinga kuchapisha mishahara yao watatozwa faini ya maelfu ya Euro.Mswaada huo wa sheria unatazamiwa kuidhinishwa na bunge la shirikisho Bundestag msimu wa mapukutiko ujao.