Wakuu wa Majeshi wa Magharibi waijadili Ukraine
2 Aprili 2025Matangazo
Akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani anayemaliza muda wake, Annalena Baerbock, Zelensky alisema hapo jana kwamba kundi dogo la nchi hizo liko tayari kutuma vikosi vyao nchini Ukraine.
Zelensky amesema mkutano huo unawajumuisha wakuu wa majeshi wa nchi yake, Ufaransa na Uingereza, mataifa mawili ambayo yameonesha utayari wa kutuma wanajeshi wake kupitia kile kinachoitwa "muungano wa wenye dhamira" ili kusimamia usitishaji mapigano unaotazamiwa kupatikana kupitia juhudi za Marekani.
Hata hivyo, Urusi inapinga kutumwa kwa wanajeshi wowote kutokea mataifa ya Muungano wa Kijeshi wa NATO. Ujerumani imeweka bayana kuwa haitoshiriki.